Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Trump Asema Marekani Itaiweka Venezuela Chini ya Usimamizi wa Mpito

  • 33
Scroll Down To Discover

Rais wa Marekani, Donald Trump

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kwamba nchi yake itaiendesha Venezuela kwa kipindi cha mpito hadi itakapohakikisha kuna uhamisho wa madaraka ulio salama, sahihi na wa busara, kufuatia operesheni ya kijeshi iliyosababisha kukamatwa kwa Rais Nicolás Maduro na mkewe Cilia Flores.

Akizungumza jana Jan. 3, 2026 katika mkutano na waandishi wa habari akiwa Mar-a-Lago, Florida, Trump alisema hatua hiyo ni muhimu ili kuunda mazingira ya amani, uhuru na haki kwa wananchi wa Venezuela. Aliongeza kwamba nchi hiyo haitarudi mikononi mwa mtu yeyote ambaye hakuangalia maslahi ya watu wa Venezuela.

Kwa mujibu wa Trump, Marekani itaweka ulinzi na usimamizi wa kisiasa wa Venezuela hadi pale itakapoweza kukabidhi madaraka kwa serikali mpya kwa njia salama na yenye

Trump pia alisisitiza kuwa hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyeuawa wala vifaa vya kijeshi kuteketea wakati wa operesheni hiyo. Alidai kuwa Maduro na mkewe watashtakiwa na kuhukumiwa chini ya sheria za Marekani kutokana na tuhuma zinazohusiana na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Halikadhalika, Trump alisema kwamba Jamuhuri ya Venezuela itakuwa chini ya usimamizi wa Marekani hadi pale itakapopatikana hali ya kisiasa imara kwa ajili ya uhamisho wa madaraka.

The post Trump Asema Marekani Itaiweka Venezuela Chini ya Usimamizi wa Mpito appeared first on Global Publishers.



Prev Post Arsenal Yaendeleza Moto Ligi Kuu England Yaichapa Bournemouth 3–2
Next Post Habari kubwa za Magazeti leo Januari 4, 2026
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook