Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Azungumza na Kaimu Balozi wa Marekani Kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo

  • 141
Scroll Down To Discover

Dodoma, Desemba 8, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, leo.

Mazungumzo hayo yamejikita katika ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa, kijamii pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa kwa kushirikiana na Marekani. Pamoja na hayo, pande zote mbili zimeeleza nia ya kuimarisha na kupanua ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, tarehe 08 Desemba, 2025.

Rais Samia alisisitiza umuhimu wa kuendeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuinua uchumi wa wananchi na kuongeza fursa za ajira, huku Balozi Lentz akionyesha msukumo wa Marekani katika kushirikiana na Tanzania kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.

Mazungumzo hayo yanajiri katika kipindi ambacho Tanzania inapanua mipaka ya ushirikiano wa kimataifa, huku ikilenga kuimarisha ustawi wa wananchi kupitia miradi ya kijamii na kiuchumi.

The post Rais Samia Azungumza na Kaimu Balozi wa Marekani Kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo appeared first on Global Publishers.



Prev Post AHMEDY ALLY ATOBOA KOCHA WA SIMBA KUJA JANUARY
Next Post Simbachawene: Hakuna Tishio la Kuzimwa Internet Tanzania, Hali ya Usalama Ni Shwari – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook