Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Breaking News: Makanisa Ya Askofu Gwajima Kufunguliwa, Agizo La Mwigulu – Video

  • 55
Scroll Down To Discover

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ameielekeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kulifungulia Kanisa la Ufufuo na Uzima, na taasisi nyingine za kidini, na iziweke chini ya uangalizi kwa miezi sita.

Aidha, ameielekeza wizara hiyo kutofungia kanisa au msikiti pindi kiongozi anapokosea kwani inaleta madhara kwa wananchi. “Akikosea Sheikh, usiadhibiwe msikiti na akikosea Askofu, wasinyimwe waumini kufanya ibada,” amesema.

Askofu Gwajima kanisa lake lilifungwa baada ya kujitokeza kupinga utekaji na mauaji yanayofanywa na ‘wasiojulikana’ huku akisisitiza kuwa hataacha kupiga kelele mambo hayo.

Kufungiwa kwa kanisa hilo kulizusha kelele nyingi kutoka kwa wananchi mbalimbali waliodai kwamba kama Askofu Gwajima amekosea achukuliwe hatua yeye na sio kuwakosesha waumini wake uhuru wa kuabudu ambao upo ndani ya katiba ya nchi.



Prev Post Serikali ya TZ yadai machafuko ya uchaguzi yalichochewa kutoka nje, katika Dira ya Dunia TV
Next Post Waziri Mkuu Mwigulu Avamia Kimara: Akagua Uharibifu wa Vurugu za Oktoba 29
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook