

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya uongozi katika Kitengo cha Mawasiliano Ikulu kwa kufanya uteuzi mpya wa viongozi wawili wapya.
Katika taarifa iliyotolewa tarehe 19 Novemba 2025 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Rais Samia amemteua Bakari Steven Machumu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.
Machumu, ambaye ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL), anachukua nafasi ya Sharifa Bakari Nyanga, ambaye amepangiwa majukumu mengine serikalini.
Katika hatua nyingine, Rais Samia pia amemteua Tido Mhando, mwanahabari mkongwe na mmoja wa viongozi wenye uzoefu mkubwa katika tasnia ya habari, kuwa Mshauri wa Rais, Habari na Mawasiliano.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa viongozi hao wataapishwa na kuanza kutekeleza majukumu yao mapya muda mfupi ujao, kulingana na utaratibu wa Ikulu.












Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!