Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Burkina Faso: Daktari Aliyekosoa Rais Traoré Atumwa Vitani Baada ya Kupata Mafunzo ya Kijeshi

  • 3
Scroll Down To Discover

Tukio lisilo la kawaida limetokea nchini Burkina Faso, baada ya daktari mmoja aliyemkosoa vikali Rais Kapteni Ibrahim Traoré kukamatwa na kupelekwa vitani kupambana na magaidi.

Daktari huyo alituhumu hadharani kuwa Rais Traoré ameshindwa kukabiliana na tishio la ugaidi linaloikabili nchi hiyo kwa muda mrefu. Hata hivyo, badala ya kufunguliwa mashitaka au kuhukumiwa, mamlaka zilimpeleka kwenye mafunzo ya kijeshi kwa miezi mitatu, kisha akapelekwa moja kwa moja kwenye uwanja wa vita.

Akizungumzia tukio hilo, Rais Traoré alisema:

“Kama kuna daktari anadhani anajua zaidi kazi ya jeshi kuliko wanajeshi, basi ni bora na yeye achangie moja kwa moja kwa kwenda vitani.”

Kauli hiyo imezua mijadala mikubwa ndani na nje ya Burkina Faso, huku baadhi wakisifu hatua hiyo kama somo la uzalendo, na wengine wakiliona kama ukiukwaji wa haki za binadamu.

Serikali ya kijeshi inayoongozwa na Kapteni Traoré imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na mashambulizi ya kigaidi yanayoendelea kaskazini mwa nchi hiyo, licha ya juhudi za kuimarisha usalama na kuhamasisha wananchi kushiriki katika ulinzi wa taifa.

LISSU ATATOBOA?/NANI KUWA WAZIRI MKUU?-MACHO YOTE BUNGENI/MARIDHIANO YATAJWA-SHIDA IKO WAPI?



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 09, 2025
Next Post Denmark Kupiga Marufuku Mitandao ya Kijamii kwa Watoto Chini ya Miaka 15
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook