
Jeneza lenye mwili wa Papa Francisko limehamishwa kutoka nyumba ya Mtakatifu Marta alipokuwa akiishi hadi kwenye Kanisa la Basilika la Mtakatifu Petro, ambapo mwili wake utatolewa heshima na waamini wote hadi mazishi yake yatakapofanyka Jumamosi tarehe 26 Aprili 2025.
Imefanyika ibada fupi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican leo Jumatano asubuhi, tarehe 23 Aprili 2024 kwa ushirikishi wa Baraza la Makardinali walioanza kukusanyika mjini Roma kufuatia kifo cha Papa Francisko kilichotokea tarehe 21 Aprili 2025.
Kardinali Kevin Farrell, Camerlengo wa Kanisa Takatifu la Roma, alianza ibada ya kiliturujia katika Kanisa Mtakatifu Marta kwa sala fupi kwa ajili ya roho ya Papa Francisko.
Katika sala ya ufunguzi, Kardinali Farrell alimshukuru mwenyezi Mungu kwa huduma ya miaka 12 ya hayati Papa Francisko. “Tunapoondoka sasa katika nyumba hii, tumshukuru Bwana kwa zawadi zisizohesabika alizowapa Wakristo kupitia mtumishi wake, Papa Francisko.
Tumwombe Yeye, kwa rehema na fadhili zake, amjalie marehemu Papa makao ya milele katika ufalme wa mbinguni, na kuwafariji kwa tumaini la kimbingu familia ya papa, Kanisa la Roma, na waamini ulimwenguni kote,” alisema.
Baadaye Baraza la Makardnaili walianza maandamano ya kuleta jeneza kupitia Uwanja wa Mtakatifu Marta wa Vatican, chini ya Tao la Kengele, na kuingia katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, kama ilivyokuwa tayari imeratibiwa.
Zaidi ya watu 20,000 walikuwa wamekusanyika katika uwanja huo kutoa heshima zao kwa marehemu Papa, wakisikika wakipiga makofi duni lakini ya kudumu wakati jeneza lake likibebwa kwenye ngazi na kuingia kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro.
Jeneza la marehemu Papa liliwekwa mbele ya madhabahu ya juu, na kwaya na wale waliokuwepo waliimba Litania ya Watakatifu kwa Kilatini kwa ajili ya kupumzika kwa roho yake.
Kisha Kardinali Farrell aliongoza Liturujia fupi ya Neno, ambayo ilijumuisha usomaji kutoka Injili ya Yohane (17:24-26) ya sala ya Yesu ya ukuhani akitangaza upendo wa Mungu kwake na kwa wanafunzi wake.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!