MAGAZETI ya Leo Jumatano 23 April 2025
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema usiku huu kimempata kwenye simu Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, John Heche na kusema taarifa zaidi zitatolewa na Heche mwenyewe kesho atakapoongea na Waandishi wa Habari.
Chadema imesema kuwa Heche ataongea na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Chama hicho kuanzia saa saba mchana na Waandishi wote wanakaribishwa.
Itakumbukwa jioni leo CHADEMA ilisema kuwa Jeshi la Polisi limemkamata Heche katika eneo la Kariakoo alikokuwa akiongea na Wananchi na baada ya kumkamata walimpeleka kituo cha Polisi Msimbazi na kisha baadae kumtoa Kituoni hapo na kusema baadhi ya Viongozi walifika kituo cha Polisi kati na kujibiwa kuwa hajafikishwa kituoni hapo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!