

Unajua kwamba mtumishi wa serikali aliyekula kiapo, akitoa siri ni kosa la jinai na anaweza kufungwa?
Omar Kashera, mshauri na mtaalamu wa uongozi wa kistratejia ambaye amebobea kwenye masuala mbalimbali ya kidiplomasia na itifaki, ameshusha nondo hizo wakati akitoa darasa kwa watumishi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha mkoani Pwani.
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram wa Omar Kashera, amekuwa akitoa masomo muhimu na kuelekeza mambo mengi ambayo wengi hawayajui kuhusu diplomasia, itifaki na uongozi.
Leo anaelezea kuhusu umuhimu wa watumishi wa serikali kutunza siri hasa wanapozungumza na simu kwani huwa wanasikilizwa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!