

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Baba Mtakatifu Francisko kilichotokea leo Aprili 21, 2025, kikimuelezea kama kiongozi aliyeamini katika haki, usawa, na utu wa binadamu.
Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Aprili 21, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, chama hicho kitamkumbuka Papa kwa kusimamia maadili ambayo yanaendana na misingi ya mabadiliko na demokrasia ya kweli.
“Alikuwa sauti ya wanyonge na mpigania mabadiliko ndani na nje ya Kanisa, akihimiza uwazi, uwajibikaji, na mshikamano wa binadamu.Tunatoa pole kwa Kanisa Katoliki, waumini wake duniani kote, na wote walioguswa na msiba huu. Tunamuombea apumzike kwa amani, huku tukiendeleza maono yake ya dunia yenye haki na utu kwa wote,”amesema.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!