Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mahakama Kuu Yakataa Ushahidi wa Flash Disk na Memory Card Kesi ya Tundu Lissu

  • 47
Scroll Down To Discover

Dar es Salaam, Oktoba 22, 2025Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imekubaliana na pingamizi la Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, na kukataa kupokea flash disk na memory card kama ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili.

Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Dustan Nduguru, kiongozi wa jopo la majaji watatu, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi. Mahakama ilisema kuwa shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka, Mkaguzi wa Polisi Samwel Kaaya (39), sio mtaalamu wa picha za mjongeo (video), bali ni mtaalamu wa picha mnato, hivyo hawanani sifa ya kutoa kielelezo hicho.

Tundu Lissu aliwasilisha sababu nne mahakamani akipinga shahidi huyo kutoa flash disk na memory card, akisisitiza kuwa haziwezi kuaminika kwa sababu shahidi hakuwa na utaalamu wa picha za mjongeo, jambo ambalo lingelenga kuthibitisha kielelezo hicho.

Mahakama ilikubaliana na hoja ya Lissu, ikikataa kupokea kielelezo hicho, jambo linaloashiria umuhimu wa kuthibitisha uhalali na sifa ya mashahidi katika kesi za uhaini nchini Tanzania.

HECHE ALIVYONYAKULIWA na POLISI MAHAKAMA KUU – ATIWA NDANI ya GARI la POLISI ULINZI MKALI….



Prev Post Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, Akamatwa na Polisi Asubuhi Hii Akiwasili Mahakamani
Next Post Rais Samia Suluhu Hassan Awapokelewa Maelfu ya Wananchi Ilala, Dar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook