MAGAZETI ya Leo Ijumaa 18 April 2025
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amebaini miradi saba ilikuwa na malimbikizo ya fidia zinazodaiwa jumla ya Sh24.75 bilioni, ikihusisha waathirika wa miradi 1,879.
CAG amebainisha hayo kwenye ripoti kuu ya mwaka ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24 baada ya kufanya mapitio kwenye miradi 360 ya maendeleo ikionyesha kutokamilishwa kwa malipo ya fidia hizo.
Kifungu cha 3(1) (g) cha Sheria ya Ardhi, Sura ya 113 kinaelekeza watu, ambao haki zao za umiliki wa ardhi zimesitishwa au kumilikiwa na serikali kulipwa kwa fidia kamili, ya haki, na kwa wakati.
Kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Utwaaji Ardhi, Sura ya 118 pia kinataka malipo ya fidia, pamoja na riba ya asilimia sita kwa mwaka kuanzia tarehe ya kumiliki ardhi hadi tarehe ya malipo, endapo ardhi itachukuliwa kabla ya malipo ya fidia kufanyika.
Katika ripoti yake, CAG amebainisha kwamba changamoto imebaki bila kutatuliwa huku baadhi ya miradi ikiwa imetekelezwa na mingine ikiwa katika hatua za kukamilika.
Miradi iliyobainishwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na Mradi wa Maendeleo ya Bonde la Msimbazi (MBDP) unaotekelezwa na Ofisi ya Rais, Tamisemi, wenye waathirika 1,034 wanaodai Sh10.9 bilioni huku hali ya utekelezaji ikiwa inaendelea.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!