

Waziri wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amesema kuwa madai ya kubadilishwa kwa mfumo wa Uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 hayawezi kutekelezwa kwa kipindi kifupi kilichobaki kwani mabadiliko makubwa yameshafanyika ikiwemo kuunda Tume huru inayojitegemea
Amesema mapungufu ya mabadiliko hayo yanapaswa kupimwa baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika.
Akizungumza Aprili 17, 2025 jijini Dodoma wakati wa kuelezea mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Simbachawene ameeleza kuwa mchakato unaogusa katiba ni suala linalohitaji muda, rasilimali, na ushirikishwaji mpana wa wananchi na sio kikundi cha watu fulani.
“Sheria zile tulipitisha pale bungeni na tukakubaliana tukanyamaza kimya, na tukasema tunaenda kwenye Uchaguzi, kama kutakuwa kuna mapungufu nadhani mapungufu yangekuja baada ya kumaliza uchaguzi huu, lakini wako wengine wanasema wao hawashiriki uchaguzi.siyo kazi yangu kuwataka washiriki uchaguzi kwa sababu ni haki ya Kikatiba
Lakini msingi na jambo la maana hapa ni kwamba je! hayo mawazo yao yanatekelezeka kwa kipindi hiki? na kama yanatekelezeka yana gharama gani?” Amesema Simbachawene
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!