Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Msemaji wa White House: Msimamo wa Trump Kuhusu Canada Haujabadilika

  • 29
Scroll Down To Discover

Rais wa Marekani Donald Trump

Msemaji wa Ikulu ya White House ametangaza kuwa Rais wa Marekani Donald Trump bado ana nia ya kuiunganisha Canada na ardhi ya nchi hiyo na kuigeuza kuwa jimbo la 51 la Marekani.

Katika wiki za karibuni, Rais Trump amepunguza mashambulizi yake ya maneno dhidi ya Canada na kuacha kutoa matamshi hadharani ya kutaka nchi hiyo iunganishwe na Marekani na kuwa jimbo la nchi hiyo.

Aidha, Trump amekuwa akimtuhumu kiongozi mpya wa Canada, Mark Carney, kama “waziri mkuu,” ilhali huko nyuma alikuwa akimwita “gavana” Waziri Mkuu wa zamani Justin Trudeau.

Pamoja na hayo, Ikulu ya White House imetangaza kuwa msimamo wa Trump kuhusu Canada haujabadilika.

Msemaji wa White House Karoline Leavitt amesema, ” Rais wa Marekani angali na msimao wake uleule kuhusu Canada. Marekani imetoa msaada wa kifedha kwa ajili ya ulinzi wa taifa wa Canada, na Donald Trump anaamini kwamba Wacanada watafaidika sana kwa nchi yao kubadilishwa kuwa jimbo la 51 la Marekani.”

Stori na Elvan Stambuli, GPL



Prev Post Global Group Tunawatakia waumini wa dini ya Kikristo Ijumaa Kuu Njema
Next Post Kikwete awasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia kwa Rais Kapteni Ibrahim Traoré
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook