MAGAZETI ya Leo Jumanne 15 April 2025
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka wananchi kutumia njia rahisi za kiteknolojia kuhakiki taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi ujao.
Akizungumza Aprili 14, 2025 na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jacobs Mwambegele, amesema kuwa wapiga kura wanaweza kuhakiki taarifa zao kwa kutumia simu ya mkononi au kutembelea tovuti rasmi ya tume.
Ameongeza kuwa huduma hiyo inalenga kuhakikisha kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura anapata nafasi ya kuhakiki taarifa zake kwa wakati kabla ya uchaguzi.
Katika hatua nyingine, Mwambegele amewakumbusha viongozi wa vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi na uboreshaji wa daftari.
Tume inaendelea na maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kupiga kura awamu ya pili, huku ikihimiza ushiriki wa wananchi kwa njia zote rasmi zilizowekwa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!