Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Samia: Serikali Italipa Kipaumbele Zao la Vanila na Miundombinu Kagera

  • 4
Scroll Down To Discover

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuunda serikali kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, ataweka mkazo maalum katika kuendeleza kilimo cha vanila wilayani Missenyi, mkoani Kagera.

Dkt. Samia amesema serikali yake itahakikisha zao hilo linatangazwa kwa upana zaidi, kupelekwa katika maonesho mbalimbali ya kilimo ndani na nje ya nchi, sambamba na kutafuta masoko ya kimataifa kwa ajili ya kuongeza thamani na kipato cha wakulima wa zao hilo.

Akizungumza leo, Jumatano, Oktoba 15, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kyaka, wilayani Missenyi, mkoani Kagera, Dkt. Samia alisema kilimo cha vanila hakijapata umaarufu mkubwa nchini kutokana na wigo mdogo wa uzalishaji na idadi ndogo ya wakulima wanaolima zao hilo.

“Soko kubwa la vanila duniani, kwa asilimia 75, linatoka nchini Madagascar, likifuatiwa na Uganda. Hivyo, hatuna sababu ya kuacha zao hili likabaki nyuma, kwani kama Uganda wanaweza, basi na sisi pia tunaweza. Tutakwenda kulitupia jicho la karibu sana zao hili la vanila,” amesisitiza Dkt. Samia.

Aidha, Dkt. Samia ametangaza mpango wa kuanza kwa ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wilayani Missenyi, mkoani Kagera, utakaokuwa na uwezo wa kuhudumia ndege kubwa aina ya Boeing zenye uwezo wa kubeba abiria kati ya 188 hadi 220.

Ameeleza kuwa kwa sasa uwanja wa ndege wa Bukoba, ambao una urefu wa kilomita 1.4, umeshindikana kupanuliwa kutokana na changamoto za kijiografia, hivyo serikali imepanga kujenga uwanja mpya mkubwa katika eneo la Kiyabajwa, wilayani Missenyi.

Kulingana na Dkt. Samia, kukamilika kwa uwanja huo kutawanufaisha wakazi wa Missenyi, mkoa wa Kagera na maeneo jirani ya Uganda, sambamba na kuongeza fursa za biashara, utalii, na kukuza sera ya kilimo-biashara katika mkoa huo wa Kanda ya Ziwa.

KILICHOTOKEA MULEBA – WENJE AJISAHAU JUKWAANI CCM ATAMKA ‘PEOPLE’S’ MBELE ya DKT SAMIA..



Prev Post Nini kinafuata baada ya mateka wa Israel na wafungwa wa Gaza kuachiliwa? Katika Dira ya Dunia TV
Next Post Wenje Ampongeza Dkt. Samia kwa Mapinduzi ya Sheria – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook