Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Samia Ahimiza uchumi wa wananchi kupitia rasilimali za madini

  • 4
Scroll Down To Discover

Bukombe, Geita — Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali ya awamu ya sita imewaruhusu wachimbaji wadogo wa madini kufanya shughuli zao ndani ya pori la akiba la Moyowosi/Kigosi, Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita, ili kuwawezesha wananchi kunufaika kiuchumi na rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Akizungumza Jumapili, Oktoba 12, 2025, mbele ya maelfu ya wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ushirombo, Dkt. Samia alisema uamuzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira yake ya kujenga utu wa Mtanzania na kuinua uchumi wa wananchi kupitia sekta ya madini.

“Vijana wangu wa Bukombe walikuwa wanaenda kuniibia madini Moyowosi/Kigosi, lakini rasilimali ile Mungu ameishusha hapa Bukombe iwafae vijana hawa. Sasa kuliko wakaibe, wakamatwe, wapigwe, wapelekwe mahakamani, nikasema hapana. Nikaagiza Biteko na wenzake wakae waone namna ya rasilimali ile kuwafaa vijana. Leo wapo hapa wanachimba, wanauza, tumewajengea masoko — na huku ndiko kujenga utu wa Mtanzania,” alisema Dkt. Samia.

Aidha, Dkt. Samia alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono wakulima wa mazao kama mahindi, mpunga na viazi kwa kutoa ruzuku za mbolea, chanjo za mifugo, pembejeo za kilimo na kuendeleza skimu za umwagiliaji, ili kukuza kilimo cha kibiashara na kuongeza pato la mkulima.

Alibainisha kuwa lengo ni kuhakikisha Watanzania wanaondokana na kilimo cha mazoea kinachotegemea mvua za msimu mmoja, na kuingia kwenye kilimo cha kisasa chenye tija kwa maendeleo ya taifa.



Prev Post BAADA YA KIPIGO CHA 4-1 JANA….PANTEV ASHTUA MASHABIKI SIMBA KWA KAULI HII…’SIWEZI….’
Next Post Waziri Mchengerwa Ataka Mabadiliko Ya Haraka Huduma Ya Usafiri Jiji La Dar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook