Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Vodacom Tanzania Yasherehekea Miaka 25 Kwa Bonanza La Michezo Arusha

  • 2
Scroll Down To Discover

Arusha, Tanzania – Vodacom Tanzania PLC imefanya sherehe ya miaka 25 toka kuanzishwa kwake kwa kuandaa bonanza la michezo jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Tukio hili lilikusanya wateja, mashabiki wa michezo na familia mbalimbali ili kusherehekea robo karne tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo.

Mpira wa miguu ulikuwa kitovu cha sherehe, huku timu ya Kuza FC ikinyakua ubingwa dhidhi ya Kitambi Noma FC baada ya kusakata kabumbu maridhawa. Kapteni wa timu hiyo Gabriel Mwandembwa, alipokea kombe kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Arusha (ARFA), Jame Rugagila.
Mbali na mpira wa miguu, Bonanza hilo pia ilijumuisha michezo ya video ya FIFA, mashindano ya gari za kuendesha kwa simu, kuvuta kamba na kukimbia huku ukiwa umevaa gunia, ikifanya tukio kuwa la kufurahisha kwa wote waliohudhuria.
Viongozi wa Vodacom,  Mkuu wa Kanda ya Kaskazini George Venanty na Meneja Masoko na Mikakati Hamida Hamad pia walishirikiana na wateja katika shughuli hizi, wakisisitiza ahadi ya kampuni ya kuendelea kuwa karibu na jamii.
Katika kusherehekea miaka 25 ya kuunganisha Watanzania, Vodacom Tanzania inaendelea kusherehekea na wateja wake kote nchini – si tu kupitia huduma bali pia kwa kutengeneza kumbukumbu za pamoja za furaha.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 19, 2025
Next Post Zelensky Yuko Tayari Kukutana na Putin, Asema Mazungumzo ni “Hatua ya Amani”
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook