NA JOHN BUKUKU MTWARA
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta ya kilimo cha korosho na sasa inashika nafasi ya pili kwa uzalishaji barani Afrika, ikitanguliwa na Ivory Coast pekee.
Dkt. Samia aliyasema hayo Septemba 26, 2025, wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Saba Saba, mjini Mtwara, ambapo alieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na mikakati ya Serikali kuimarisha kilimo cha korosho kupitia upatikanaji wa pembejeo, utafiti, na ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya wakulima.
Alisisitiza kuwa korosho siyo tu zao la biashara, bali pia linabeba ajira kwa maelfu ya Watanzania hususan katika mikoa ya kusini, na kuahidi kuendeleza mapinduzi ya kilimo ili kuongeza thamani na kipato kwa wakulima.
“Leo hii Tanzania ni ya pili Afrika kwa uzalishaji wa korosho. Hii ni hatua kubwa inayothibitisha dhamira yetu ya kuwekeza kwenye kilimo, na ninaahidi endapo mtatupa ridhaa ya kuendelea kuongoza kwa kutupigia kura ya ndito kwa Rais, Wabunge na Madiwani itakapofika Oktoba 29, 2025 tutazidi kuimarisha mnyororo mzima wa thamani ya korosho,” alisema Dkt. Samia huku akishangiliwa na umati wa wananchi katika mkutano huo.
Aliwahiniza wana CCM na wananchi mbalimbli kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya uchaguzi na kukipigia kura Cha Cha Mapinduzi CCM ili kikawaletee maendeleo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!