Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Ushuru mpya wa Trump watikisa masoko ulimwenguni

  • 8
Scroll Down To Discover

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza ushuru mpya kwa bidhaa zote zinazoingia nchini humo, kiwango cha chini kikiwa asilimia 10, huku baadhi ya nchi zikikabiliwa na ushuru wa hadi asilimia 50.

Umoja wa Ulaya utatozwa asilimia 20, Japan asilimia 24, Mexico na Canada asilimia 25 iliyowekwa awali, India asilimia 26, China asilimia 34, huku nchi maskini kama Vietnam na Mynmar zitatozwa hadi ushuru wa asilimia 50.

Trump amesema ushuru huo unalenga kushughulikia miaka mingi ya biashara isiyo ya haki ambayo imeathiri Marekani. Ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa zote utaanza kutumika tarehe 5 Aprili, mwaka huu.

“Tutaifanya Marekani kuwa kubwa na tajiri tena. Nchi yetu imenyang’anywa kwa zaidi ya miaka 50. Hilo halitafanyika tena,” amesema.

Hatua hiyo imeleta mtikisiko katika masoko ya dunia, huku masoko ya Asia yakishuka kwa kasi.

The post Ushuru mpya wa Trump watikisa masoko ulimwenguni appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post Serikali yaahidi kushirikiana na wadau kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini
Next Post Kampuni ya xAI yaununua mtandao wa X
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook