
Msemaji Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amesema kuwa ujenzi wa Kongani ya Viwanda ya Sino-Tan Kibaha (Industrial Park) katika eneo la Kwala, mkoani Pwani, unaendelea, na utakapokamilika utakuwa na viwanda vikubwa 200 na viwanda vidogo 300.
Viwanda hivyo vitajumuisha sekta mbalimbali, zikiwemo usindikaji wa chakula, kemikali, nguo, na dawa.
Msigwa amesema kongani hiyo inatarajiwa kutoa zaidi ya ajira laki moja za moja kwa moja na ajira zisizo za moja kwa moja laki tano.
Video Nzima ipo katika Akaunti yetu ya youtube ya Bongo5
Written edited by #abbrah255 and @el_mando_tz
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!