

Jeshi la Polisi nchini linatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi kuanzia Agosti 11 hadi 15, 2025 katika Shule ya Polisi Tanzania – Moshi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi pamoja na kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha na kudumisha usalama nchini ikiwemo ya kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unafanyika katika mazingira yenye amani, utulivu na usalama.
Mkutano huo, unatarajiwa kufunguliwa na Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 11, 2025.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime amesema Katika Mkutano huo pamoja na kufanya tathmini, mada mbalimbali zitawasilishwa kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!