Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kesi ya CHADEMA Kusikilizwa Agosti 18, Mahakama Kutoa Uamuzi wa Zuio

  • 49
Scroll Down To Discover

Kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu wa chama hicho, inayohusu zuio la kufanya shughuli za kisiasa, imeahirishwa hadi Agosti 18, 2025, kwa ajili ya kusikilizwa kwa uamuzi wa maombi ya kutengua zuio hilo.

Shauri hilo, Na. 8323/2025, liliwasilishwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA upande wa Zanzibar, Said Issa Mohammed, na linahusu zuio lililotolewa na Mahakama tarehe 10 Juni 2025, ambalo liliwazuia viongozi wa CHADEMA kufanya shughuli za utendaji pamoja na kutumia rasilimali za chama.

Katika hatua ya hivi karibuni, upande wa walalamikiwa kupitia kwa mawakili wao wamewasilisha maombi ya kutaka zuio hilo litenguliwe, wakidai kuwa lilienda kinyume cha haki ya kikatiba ya kushiriki siasa. Pia wameeleza kuwa wakati zuio hilo linatolewa, hawakuwa na mwakilishi mahakamani baada ya Wakili Jebra Kambole kujitoa, hivyo walinyimwa haki ya kusikilizwa.

Hata hivyo, upande wa wajibu maombi umepinga hoja hizo kwa msingi kuwa walalamikiwa hawakukosa haki ya kusikilizwa, bali walishindwa kufuatilia mwenendo wa shauri hilo kwa uzembe wao wenyewe.

Mahakama imesema itatoa uamuzi kuhusu hoja hizo tarehe 18 Agosti, hatua ambayo itaamua kama zuio hilo litaendelea kuwepo au la.



Prev Post NAFASI Za Kazi Azam Media, Ajira Mpya Azam TV
Next Post Utalii Wafunga Mwaka 2024/25 Ukiongoza Fedha za Kigeni
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook