Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

CAG: DENI LA SERIKALI BADO NI HIMILIVU

  • 10
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 kutoka kwa Bw. Charles Kichere, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 30 Machi, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 30 Machi, 2026.

Na. Fullshangwe Blog – Dar es salaam

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dkt. Charles Kichere, Machi 30, 2026, amewasilisha Ripoti Kuu ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa deni la Serikali bado ni himilivu na lipo ndani ya viwango salama vinavyokubalika kimataifa.

Aidha amebainisha kuwa thamani ya sasa ya deni lote la umma kwa Pato la Taifa ni asilimia 40.7, ikiwa chini ya ukomo wa asilimia 55, huku deni la nje kwa Pato la Taifa likiwa ni asilimia 24.9 chini ya ukomo wa asilimia 40.

Amesema kuwa deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 125.5, ambalo bado lipo ndani ya kiwango cha asilimia 180.

Aidha amebainisha kuwa deni la Serikali limefikia Shilingi trilioni 110.05 kutoka Shilingi trilioni 97.35.

Amesema kuwa deni hilo linajumuisha deni la ndani la Shilingi trilioni 35.5 na deni la nje la Shilingi trilioni 74.55.

Aidha amebainisha kuwa mwenendo huo unaonesha kuwa ndani ya mwaka mmoja deni limeongezeka kwa Shilingi trilioni 12.73 ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2023/2024.

Amesema kuwa ongezeko hilo limechangiwa zaidi na kuongezeka kwa mikopo ya nje pamoja na kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani.

Aidha amebainisha kuwa kushuka kwa thamani ya shilingi kumechangia ongezeko la deni la Shilingi trilioni 2.

Amesema kuwa ukuaji wa uchumi umeimarisha uaminifu wa Tanzania kimataifa, jambo linaloonekana kupitia ukadiriaji wa hadhi ya ukopaji ambapo nchi imepata daraja la B, huku mwezi Desemba Fitch Ratings ikitoa daraja la B+ mwezi Machi mwaka huu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 30 Machi, 2026.



Prev Post Kampuni ya Bia ya Serengeti Yazidi Kuonesha Uaminifu wa Kuendeleza Ukuaji wa Viwanda kwa Ushirikiano na Wizara ya Viwanda na Biashara
Next Post TAASISI YA KIMATAIFA YA FISCH YATABIRI UIMARA UCHUMI WA TANZANIA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook