Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Bunge la Iran Lapitisha Kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz

  • 44
Scroll Down To Discover

Tehran, Iran – Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limepitisha kwa kura nyingi muswada wa kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz, hatua ambayo imeleta mshituko mkubwa kwenye soko la nishati duniani na kuongeza hofu ya kuongezeka kwa mivutano ya kijeshi katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Spika wa Bunge la Iran alitangaza rasmi uamuzi huo Juni 22, 2025 akieleza kuwa hatua hiyo ni jibu kwa kile kinachoitwa uchokozi wa mara kwa mara kutoka kwa mataifa ya Magharibi, hususan Marekani.

Mbunge mmoja mwandamizi alisisitiza kuwa, Iran ina haki ya kujilinda dhidi ya vitisho vya kigeni, na hatua hii ni ya kimkakati kwa usalama wa taifa letu na maeneo ya jirani.

Mlango-Bahari wa Hormuz hupitisha takriban 20% ya mafuta yote ghafi yanayouzwa kimataifa, na kufungwa kwake kunatarajiwa kupandisha bei ya mafuta kwa kiwango kikubwa na kutatiza biashara ya kimataifa.

Jumuiya ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa na Muungano wa Ulaya wametoa wito kwa Iran kujizuia na kuchagua njia ya kidiplomasia, wakionya kuwa hatua hiyo inaweza kusababisha machafuko ya kimataifa na kuvuruga amani ya kikanda.

Hatua ya Iran inakuja katika kipindi cha ongezeko la mivutano baina yake na Marekani, huku wachambuzi wakiona hali hii kama “cheche mpya” inayoweza kuwasha moto mkubwa katika eneo hilo la kimkakati duniani.



Prev Post Iran Yatoa Onyo Kufuatia Mashambulizi ya Marekani Kwenye Vituo vya Nyuklia
Next Post Jeshi La Iran: Marekani Na Israel Zisubiri Majibu Ya Majuto
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook