
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 06 June 2025
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 06 June 2025
Wanachama wa Klabu Yanga ambao ni viongozi wa Matawi, wametoa Msimamo mkali wakiwataka mashabiki wa timu hiyo kutobabaishwa kwani kikosi chao hakitakwenda uwanjani kwenye mchezo wa Dabi ya Kariakoo, Juni 15, 2025.
Msimamo huo umetolewa leo na Mratibu wa Matawi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shabani Mgonja, aliyebainisha kuwa Baraza la Matawi limepitisha uamuzi rasmi kwamba hawatashiriki mchezo huo.
Mgonja ameonya kuwa endapo Simba SC, Bodi ya Ligi na Waamuzi watajitokeza kwa ajili ya mchezo huo na ikatolewa uamuzi wa Yanga kunyang’anywa pointi 15, basi kwao itakuwa mwisho wa ushiriki katika Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kuwa hawana tena imani na uongozi wa Bodi ya Ligi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!