
MAGAZETI ya Leo Jumatano 28 May 2025
MAGAZETI ya Leo Jumatano 28 May 2025
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limewaita vijana waliomaliza kidato cha sita mwaka 2025 kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2025.
Kwa mujibu wa JKT, vijana hao wanatakiwa kufika katika makambi waliyopangiwa Kuanzia May 28 hadi June 8, 2025.
Vijana hao wamepangiwa kuripoti katika makambi ya JKT Rwamkoma (Mara), Msange (Tabora), Ruvu na Kibiti (Pwani), Mpwapwa na Makutopora (Dodoma).
Kambi nyingine za JKT ni Mafinga (Iringa), Mlale (Ruvuma)Mpambo na Maramba (Tanga), Makuyuni na Orjolo (Arusha), Bulombora, Kanembwa na Mtabila (Kigoma), Itaka (Songwe) Luwa na Milundikwa (Rukwa), pamoja na Nachingwea (Lindi).
Aidha Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu iliyo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!