

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, Agosti 14, 2025, amemkabidhi fomu za uteuzi wa kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mgombea wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Elias Mulumbe.
Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za Tume, zilizopo Njedengwa, jijini Dodoma.
Mulumbe aliambatana na mgombea mwenza wa kiti cha Makamu wa Rais kwa tiketi ya ADC, Mhe. Shoka Khamis Juma.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!