Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MC Mwingira, Msanii wa Nyimbo za Hamasa CHADEMA, Afariki kwa Ajali ya Gari

  • 5
Scroll Down To Discover

Msanii wa Nyimbo za Hamasa za CHADEMA, ‘MC Mwingira’ George Mwingira

Mtunzi na mwimbaji wa nyimbo mbalimbali za hamasa za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akiwemo wimbo maarufu “Tundu Lissu Wapeleke Mchakamchaka”, George Mwingira amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kusini, Belle Ponera, Mwingira alifariki dunia Jumapili, Agosti 10, 2025, katika eneo la Mikumi, mkoani Morogoro, baada ya basi alilokuwa akipanda kutoka Songea (Ruvuma) kuelekea Dar es Salaam kupata ajali.

Mbali na wimbo huo, Mwingira maarufu kama MC Mwingira aliwahi pia kutamba na kibao cha “No Reforms No Election”, ambacho ndicho kilikuwa kazi yake ya mwisho kabla ya kifo chake.

Kifo chake kimeendelea kuwa pigo kwa CHADEMA kwa kuwapoteza wasanii wake wa nyimbo za hamasa, ambapo kabla yake walifariki dunia:

Fulgence Mapunda ‘Mwanacotide’ (2019), aliyeimba “Chadema People’s Power” na “Polisi Msitupige Mabomu Chadema”.

Sara Alex (2022), aliyeimba wimbo “Mwamba Tuvushe”.



Prev Post Luhaga Mpina Kuchukua Fomu ya Kugombea Urais Leo Dodoma
Next Post Mgombea Urais wa CUF, Gombo Samandito, Akabidhiwa Fomu na NEC
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook