Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Uhusiano wa Ruto na Raila Wazua Hali Tete, Gachagua Aingia Kati

  • 6
Scroll Down To Discover

Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua

Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amemshambulia vikali kwa maneno kinara wa chama cha ODM Raila Odinga akimuelezea kuwa ni mwanasiasa anayewania urais bila kuutaka wadhifa huo.

Gachagua, ambaye yupo nchini Marekani akiendelea na ziara ya miezi miwili ya kukutana na Wakenya wanaoishi huko amedai kuwa, Raila ni mtu anayetaka mamlaka bila uwajibikaji na ndio maana amekuwa (akiwahadaa wafuasi wake wamfuate lakini akifika debeni huhakikisha anashindwa kwa kutumia mbinu zote.

Gachagua amesema: “kila uchaguzi Raila amekuwa akiwatumia binamu kutoka Ukambani, Mulembe, Taita, Kisii, Mijikenda na anawadanganya anawapeleka Canaan. Kwa sababu binamu wanataka kuingia huko wanamfuata. Akiingia huko hataki kuwa rais, anataka tu mamlaka bila uwajibikaji. Anazua ghasia ili ajiunge na serikali kisha anaanza kula na kunyamaza akisubiri uchaguzi mwingine kuwahadaa tena”.

Naibu rais huyo wa zamani wa Kenya amesisitiza kuwa siasa za Raila zimeisha na kazi yake ni ‘kula serikalini’ akiwa amenyamaza.

Gachagua ametoa matamshi hayo makali wakati uhusiano kati ya Raila na Rais wa Kenya William Ruto umeonekana kunoga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

Ijumaa iliyopita, Raila aliwakemea vikali wale wanaosema Rais Ruto anastahili kuhudumu kwa muhula mmoja pekee, akisema hilo litaamuliwa na Wakenya kutokana na utendakazi na uwajibikaji wa serikali ya sasa.



Prev Post CCM Kongwa Kuanzisha Upya Zoezi la Kuchukua Fomu za Ubunge Baada ya Kifo cha Ndugai
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 13, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook