Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

WAHASIBU WA TAASISI ZA UMMA WATAKIWA KUWA MABALOZI WA KODI

  • 43
Scroll Down To Discover

 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amewataka wahasibu wa taasisi za Umma kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari. 

Ameyasema hayo leo tarehe 01.08.2025 akifungua semina kwa wahasibu kutoka taasisi mbalimbali za Umma nchini juu ya madaliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. 

Bw. Mwenda amesema kuwa Wahasibu wa sekta wa Sekta ya Umma wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika ulipaji wa kodi, kutoa taarifa za ukwepaji wa kodi na kuwaelimisha wengine kulipa kodi kwa wakati ili kuiwezesha serikali kuendelea kutekeleza shughuli za maendeleo kwa wakati. 

“Ninyi munatakiwa muwe mstari wa mbele kulipa kodi na muwe walimu wa kuwafundisha wengine kulipa kodi.”

Aidha, amewahakikishia washiriki hao TRA kuendelea kutoa ushirikiano katika kutimiza wajibu wao ikiwa pamoja na kusikiliza changamoto zao na kuzitatua. 

Pia, amewaahidi washiriki hao kuwa TRA itaendelea kutoa huduma bora sambamba na kuboresha mifumo ya kodi ili waendelee kulipa kodi kwa urahisi zaidi.



Prev Post Miaka 25 ya Vodacom: Kuadhimisha Uunganishwaji Kidijitali
Next Post STANBIC YAANDAA JUKWAA LA KIHISTORIA KUHUSU UWEKEZAJI NA UHAMASISHAJI MITAJI UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook