
Na Mwandishi Wetu,Manyara.
Benki ya NMB imesema itaendelea kutoa huduma bora kwa Walimu ikiwemo kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha kujiendeleza kiuchumi na kijamii ili kuhakikisha ustawi wa kundi hilo muhimu kwenye jamii.
Hayo yamesemwa na Meneja mwandamizi Wa wateja Binafsi Wa Beki ya NMB Ally Ngingite wakati akizungumza na walimu Wa wilaya ya Babati Mkoani Manyara Katika Bonanza la Mwalimu Spesho inayoandaliwa na Benki hiyo kila mwaka ambapo amesema wataendelea kutoa mikopo ya haraka kwa walimu ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Mkuu Wa Idara ya Wateja Binafsi Benki ya NMB Aikasia Muro amesema bonanza hilo ambalo linafanyika kwa mwaka wa kumi sasa ni maalum kwa ajili ya kuwakutanisha walimu na kuwapatia masuluhisho ya huduma za kibenki ikiwemo mikopo yenye riba nafuu pamoja na huduma nyingine nyingi ambazo ni rafiki kwa walimu.
Mgeni Rasmi katika Bonanza hilo Kaimu Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Mji Babati Gasto Silayo amesema walimu wameendelea kunufaika kupitia benki hiyo na ushirikiano ni mkubwa kati ya benki hiyo na Serikali kutokana na huduma bora wanayotoa kwa wateja wake
Baadhi ya walimu wilayani humo wameishukuru Benki hiyo kwa kuwarahisishia baadhi ya mambo kupitia mikopo wanayotoa kwa walimu hivyo wamewaomba walimu wengine kujiunga na Benki hiyo ili kufaidi matunda yanayopatikana katika benki hiyo kwa kuwaleta watu karibu
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!