Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

JWTZ Latoa Msaada, Ujenzi wa Nyumba za Manusra Nchini Rwanda

  • 30
Scroll Down To Discover

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limetoa msaada wa maboksi mia moja ya vigae na matenki matano yenye ujazo wa lita elfu kumi kila moja kama mchango wake katika ujenzi wa nyumba nane zilizopo Wilaya ya Karongi nchini Rwanda, kwaajili ya manusura wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda,Mkurugenzi wa Tiba wa JWTZ Brigedia Charles Emilio Mwanziva amesema kuwa pamoja na kukabidhi vifaa hivyo,pia JWTZ limetoa wataalam wa Tiba ambao wameungana na wengine kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kushiriki kutoa huduma kwenye hospitali na vituo vya afya mbalimbali nchini humo ikiwa ni sehemu ya mpango wa Majeshi ya Jumuiya kuimarisha uhusiano wao na wananchi kwenye nchi wanachama.

Naye Meya wa Mji wa Karongi Mheshimiwa Kazungu amelishukuru JWTZ kwa msaada lililoutoa huku akiainisha kuwa mpango wa kuwapatia makazi bora manusura hao unafanyika nchi nzima kwa kuzingatia matumizi bora ya ardhi ili kuhakikisha wananchi wanapata maeneo kwaajili ya shughuli za Kilimo huku Serikali ikitenga maeneo ya uwekezaji ili kukuza uchumi wa Taifa hilo.

Amesifu mpango wa Majeshi ya EAC katika kuhakikisha kuwa yanashiriki shughuli za kimaendeleo kwani kwa kufanya hivyo yanawafanya wananchi kuwa karibu nayo na kutoa ushirikiano mkubwa pindi wanapowahitaji.

Tukio la kukabidhi misaada hiyo limefuatiwa na uzinduzi nyumba hizo ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi anayehusika na Serikali za Mitaa Nchini Rwanda Mheshimiwa Maria Sorange Kaisire

EAST AFRICA CIVIL MILITARY COOPERATION ACTIVITIES ni mpango uliobuniwa na Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii na kujenga mahusiano mazuri kati ya Majeshi na raia ambapo hii ni mara ya tano shughuli hizo kufanyika ambapo hufanywa kwa mzuguko ndani ya nchi wanachama.

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.



Prev Post NAFASI Za Kazi CVPeople Tanzania
Next Post Shigongo: Umoja Ndio Njia Pekee ya Kuinua Buchosa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook