Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mazishi ya Wanandoa wa Bonyokwa Kufanyika Juni 18 Kilimanjaro, Watahifadhiwa Pamoja – Video

  • 40
Scroll Down To Discover


Nuhu Msangi, msemaji wa familia ya wanandoa waliokutwa wamefariki dunia ndani ya chumba chao usiku wa kuamkia Juni 12, 2025, katika mtaa wa GK, Bonyokwa, jijini Dar es Salaam wakiwa na majeraha mbalimbali mwilini, ametoa ratiba ya mazishi ya wawili hao.

Amesema kuwa wanandoa hao watahifadhiwa sehemu moja, upareni siku ya jumatano Juni 18, 2025 wakipumzishwa pamoja kama walivyoishi pamoja enzi za uhai wao.

Akizungumza wakati akitoa ratiba hiyo, Msangi amelishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano mkubwa walioutoa tangu mwanzo wa tukio hilo hadi kufanikisha familia kuweza kukamilisha maandalizi ya kuwapumzisha wapendwa wao kwa amani.

Pia amewashukuru ndugu, jamaa na marafiki kwa kuwa karibu na familia katika kipindi hiki kigumu huku akiwaomba waendelee kuwa nao bega kwa bega hadi pale wanandoa hao watakapopumzishwa rasmi.



Prev Post Mazishi ya Wanandoa wa Bonyokwa Kufanyika Juni 18 Kilimanjaro, Watahifadhiwa Pamoja – Video
Next Post Majaliwa Mgeni Rasmi Maadhimisho Miaka 21 Ya TAHLISO
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook