Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 13 June 2025

  • 15
Scroll Down To Discover

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 13 June 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 13 June 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 13 June 2025

Ndege ya Shirika la Ndege la Air India iliyokuwa ikielekea jijini London nchini Uingereza imeanguka katika eneo la makazi la Meghani Nagar nchini India ikiwa na jumla ya abiria na wahudumu 242.

Ndege hiyo inadaiwa kudondoka ardhini muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Ahmedabad Saa 7:38 mchana leo Alhamisi, Juni 12, 2025.

Shirika la Habari la Reuters limeripoti leo Alhamisi Juni 12, 2025, kuwa inahofiwa kwamba kuna vifo na majeruhi wengi katika ajali hiyo.

Ndege hiyo ya Air India aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, ilikuwa na abiria 230 na wahudumu 12, wakiwemo Rubani Mkuu, Sumit Sabharwal na Rubani Msaidizi, Clive Kunder.

Ndege hiyo, iliyopaa kutoka uwanja wa Ahmedabad Saa 7:38 mchana, ilikuwa na jumla ya watu 242 ndani. Miongoni mwao, 169 ni raia wa India, 53 wa Uingereza, mmoja wa Canada na 7 wa Ureno.

Kulingana na Kituo cha Udhibiti wa Polisi, ndege hiyo ya Air India yenye nambari ya safari AI 171 ilikuwa ikielekea London nchini Uingereza.

“Mnamo Juni 12, 2025, ndege ya Air India B787 yenye usajili VT-ANB, ikiwa katika safari ya AI-171 kutoka Ahmedabad kwenda Gatwick (London), ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Ahmedabad,” imesema taarifa ya mamlaka hiyo.



Prev Post Umma Usipotoshwe Kuhusu Kesi ya Chadema : Mawakili wa Mdai
Next Post Taarifa Ya Polisi Ajali Iliyoua Watu 9 Na Kujeruhi 44, Kamanda Afunguka Ajali – Video
Related Posts
© Image Copyrights Title

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 12 June 2025

© Image Copyrights Title

MAGAZETI ya Leo Jumatano 11 June 2025

Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook