
MAGAZETI ya Leo Jumatano 11 June 2025
MAGAZETI ya Leo Jumatano 11 June 2025
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imezuia kwa muda shughuli zote za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katibu mkuu, mawakala na wafuasi wa chama hicho kushiriki kwa namna yoyote hadi pale kesi ya msingi itakaposikilizwa.
Pia, imeagiza mali zote za Chadema zisitumike mpaka pale kesi ya msingi itakaposikilizwa.
Kesi ya msingi kuhusu mgawanyo wa rasilimali za chama hicho imepangwa kuanza kusikilizwa Juni 24, 2025.
Kesi hiyo imefunguliwa na Said Issa Mohamed, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Zanzibar na wenzake wawili, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu, ambao ni wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chadema kutokea Zanzibar.
Wadaiwa katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Hamidu Mwanga ni Bodi ya Wadhamini wa Chadema, ikiwa mdaiwa wa kwanza na Katibu Mkuu wa Chadema, akiwa mdaiwa wa pili.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!