Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Madereva Wa Serikali Arusha Wapatiwa Mafunzo Kujengewa Uwezo

  • 28
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha limetoa mafunzo kwa madereva wanaondesha magari ya Serikali mkoani humo kwa ajili ya kuwajengea uwezo juu ya matumizi sahihi ya barabara sambamba na matumizi sahihi ya mifumo ya Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani humo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema mafunzo hayo ni muendelezo wa kuyafikia makundi mbalimbali katika jamii kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika kukabiliana na ajali za barabarani na kufahamu mifumo mipya ya Jeshi la Polisi katika kufuatilia haki zao.

SSP Zauda amebainisha kuwa Jeshi la Polisi linamifumo mingi katika kutekeleza majukumu yake ambapo madereva wamepata fursa ya kujifunza mifumo mbalimbali ikiwemo mfumo wa ukaguzi wa magari, mfumo wa leseni na mfumo wa ukaguzi wa madeni ya Serikali.

Aidha amesema kupitia mafunzo hayo madereva hao wataenda kubadilika na kuwa mabalozi wazuri wa usalama barabarani na kutoa wito kwa madereva wengine kuhakikisha wanatii na kufauta sheria za usalama barabarani.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa OSHA kanda ya Kaskazini Bw. Abubakari Shabani amesema katika mafunzo hayo wamepata fursa ya kutoa elimu juu ya umuhimu wa kupima afya hususani macho ambapo madereva wengi wamejitokeza kupima macho yao ambapo amesema itasaidia kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na changamoto ya macho.

Naye Afisa wa Mazingira toka wakala Barabara TANROAD Mkoa wa Arusha Bw. Gabriel amesisitiza umuhimu wa madereva kufuata alama za barabarani ikiwemo vivuko vya watembea kwa miguu, maeneo ya maegesho sambamba na maeneo ya kugeuzia magari ili kuepusha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.

Nao baadhi ya madereva waliopata mafunzo hayo wameeleza kufurahishwa na elimu waliyoipata kwani inawasaidia kuwakumbusha mabadiliko mbalimbali ya mifumo na sheria za usalama barabarani na kutoa rai kwa madereva wengine pindi wanaposikia uwepo elimu kama hiyo kujitokeza kwa wingi.



Prev Post Mapinduzi ya Kijani ya Meridianbet: Miradi 80 ya Uendelevu Katika Robo ya Kwanza ya 2025.
Next Post Chukua Chako Mapema na Meridianbet Leo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook