Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Benki ya Exim Tanzania Yaleta ‘Elite Banking’ Arusha na Kilimanjaro

  • 10
Scroll Down To Discover

Baada ya uzinduzi wa huduma ya Elite Banking jijini Dar es Salaam, Benki ya Exim sasa yasogeza huduma hii kwa wateja wake wa Arusha na Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kutoa huduma bora na za kipekee kwa wateja wake kote Tanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Shani Kinswaga,“Kiini cha uzinduzi huu kilikuwa ni kuanzishwa kwa falsafa mpya ya ‘Kufafanua Upya Dhana ya Upekee’.

Huduma hii siyo tu ya kifedha, bali ni ahadi yetu ya kuwapa wateja huduma zinazoendana na mahitaji na ndoto zao. Kupitia suluhisho bora za kifedha, ushauri wa kitaalamu, pamoja na timu maalum ya wasimamizi wa mahusiano, Elite Banking inakuja na kiwango kipya cha huduma ya kisasa na rahisi. Kusogeza huduma hii Arusha na Kilimanjaro ni sehemu ya maono yetu ya kuhakikisha wateja wetu wote nchini wanapata huduma za kipekee na za kisasa.”

Aliongezea kuwa Elite Banking inazingatia nguzo kuu tatu: Ubora wa hali ya juu, huduma za kipekee, na Urahisi. Ubora wa kipekee unaokuja na viwango vipya katika huduma za kibenki kwa kuwasogezea wateja wetu ulimwengu wa huduma za kidigitali karibu zaidi popote walipo duniani, fursa za maisha na suluhisho za kifedha. Huduma ya kipekee yenye timu maalum ya usimamizi wa mahusiano na mteja anaweza kufurahia maeneo maalum ya mapumziko. Urahisi na usisamizi wa kifedha usio na usumbufu.

“Hii siyo tu huduma ya kawaida ya kibenki, bali ni huduma maalum na ya kipekee iliyobuniwa kwa ajili ya kutambua mahitaji ya mteja na kusaidia mteja kutimiza ndoto na malengo yake ya kifedha”

Uzinduzi huu unajengwa juu ya msingi imara uliowekwa na huduma ya ‘Preferred Banking’ iliyoanzishwa mwaka 2016, na sasa unavuka mipaka kwa kutoa suluhisho za kibenki za kipekee kwa haraka na kwa ubora zaidi, Benki ya Exim inajivunia kuwaletea wateja wake huduma hii ya Elite Banking.

Elite Banking inajumuisha faida mbalimbali kama vile sehemu maalum za mapokezi ndani ya matawi, usafiri wa kimataifa kupitia Mastercard, ushauri wa kifedha binafsi, na mipango ya kifedha iliyoundwa kulingana na malengo ya mteja. Kila mteja anapata Meneja wa Mahusiano anayetoa ushauri kulingana na mahitaji ya mteja.

Bw. Andrew Lyimo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Rejareja katika Benki ya Exim, aliongezea “Elite Banking iliundwa kwa lengo la kuwapatia wateja wetu safari ya kibenki inayolingana na malengo yao. Kwa kuunganisha wateja na ubora wa kipekee, huduma zilizorahisishwa,fursa mbali mbali zinazolenga kumwezesha mteja kwa ujumla.

Benki ya Exim imeungana na Mastercard kuleta Mastercard World Card Suite inayojumuisha kadi tatu: Mastercard World Debit Card (TZS), Mastercard World Debit Card (USD), na Mastercard World Credit Card. Kila kadi imeundwa kutoa urahisi wa kimataifa, na suluhisho za kifedha zinazokidhi mahitaji ya wateja.

Bw. Andrew Lyimo aliongezea kuwa ushirikiano huu na Mastercard unakuja na manufaa mengi ikiwemo urahisi wa kupata maeneo maalum ya kusubiria kwenye viwanja vya ndege kote duniani (DragonPass) zaidi ya 1,000 duniani, huduma maalum za kipekee na huduma za usafiri wa kifahari, pamoja na bima kamili ya kusafiri inayojumuisha kila kitu kuanzia ajali hadi matibabu ya dharura. Wamiliki wa kadi hizi pia wanapata ulinzi thabiti wa manunuzi duniani kote, pamoja na zawadi za kipekee kwa ajili ya manunuzi, milo, usafiri, na burudani, zote zikiendeshwa na teknolojia ya kisasa ya malipo isiyotumia fedha taslimu.

Kwa kuileta Elite Banking, Benki ya Exim inathibitisha nafasi yake kama mshirika wa kuaminika katika safari za kifedha, ikileta upekee kupitia huduma za kibinafsi, zinazohusiana na mahitaji, na zenye manufaa ya kweli.

Zaidi ya urahisi wa matumizi, Wamiliki wa kadi pia hufurahia ulinzi imara wa ununuzi wa kimataifa, Mifumo ya hali ya juu ya kuzuia ulaghai, na program za kipekee za zawadi zilizoundwa mahsusi kwa ajili ya chakula, manunuzi,usafiri na burudani.Huduma hii ina teknolojia ya kisasa ya malipo bila kugusa, Mastercard World card Suite inahakikisha kila muamala ni salama,rahisi na wa kipekee ambayo ni msingi na lengo kuu la Elite Banking

Mwisho.

Kuhusu Exim Bank Tanzania

Exim Bank Tanzania ni mojawapo ya taasisi za kifedha zinazoongoza nchini, inayojulikana kwa uvumbuzi unaomlenga mteja, uaminifu, na kuvuka mipaka nje ya Tanzania. Benki inaendelea kuweka viwango vipya katika huduma za kisasa za kibenki ikiwa na huduma zinazokua kwa kasi.

Kuhusu Mastercard

Mastercard ni kampuni ya teknolojia ya kimataifa katika sekta ya malipo. Dira yake ni kuunganisha na kuwezesha uchumi jumuishi wa kidijitali unaowanufaisha wote, kila mahali, kwa kufanya miamala kuwa salama, rahisi, haraka, na yenye kufikiwa kwa urahisi.

The post Benki ya Exim Tanzania Yaleta ‘Elite Banking’ Arusha na Kilimanjaro appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post Mtanzania Adaiwa Kuuawa na Polisi Afrika Kusini, Familia Yalia Uchungu – Video
Next Post Balozi Nchimbi Ahamasisha Maelfu Kumsapoti Dkt. Samia Itilima
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook