
Wananchi wa Kata ya Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma, leo wamejitokeza kwa wingi kufuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi, Dkt. Samia aliwasilisha sera na ahadi zinazolenga kuimarisha sekta za kilimo, afya, elimu na miundombinu, akisisitiza kuwa serikali itakayoundwa na CCM itaendelea kushughulikia changamoto za wananchi kwa vitendo.
Wananchi walionekana kufuatilia hotuba yake kwa makini, huku wengine wakishangilia na kuonesha ishara za kumuunga mkono katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!