Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makamu Wa Rais Afanya Mazungumzo  Na Balozi  Wa Ghana Nchini Tanzania

  • 1
Scroll Down To Discover

Asisitiza umuhimu wa  Ushirikiano zaidi wa  kiuchumi  baina  ya Mataifa  mawili
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Ghana nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mhe. Damptey Bediako Asare, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amesema Tanzania na Ghana zimeendelea kunufaika na uhusiano uliopo wa kihistoria ulioanza tangu kipindi cha utafutaji uhuru wa mataifa hayo ukichagizwa na urafiki wa Baba wa Mataifa hayo, Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Baba wa Taifa la Ghana hayati Kwame Nkurumah. Amesema Tanzania inatambua mchango wa Jamhuri ya Ghana katika ukombozi wa Mataifa ya Kusini mwa Afrika wakati wa kupigania uhuru.
 Makamu wa Rais amesema mataifa hayo mawili yameendeleza ushirikiano uliopo ambapo kwa sasa yamejikita zaidi katika mahusiano ya kiuchumi. Ameongeza kwamba ni muhimu kuendelea kushirikiana zaidi katika uwekezaji na biashara kupitia mpango wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCTFA). Aidha amesema ushirikiano zaidi unahitajika katika sekta mbalimbali kama vile sekta ya madini, kilimo, utalii, TEHAMA, elimu na huduma za jamii. Amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Ghana kuwekeza nchini Tanzania kupitia fursa nyingi zilizopo.
Pia Makamu wa Rais ameipongeza Ghana kwa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam mwaka 2024. Amesema kupitia maonesho hayo, ushirikiano wa kiuchumi baina ya mataifa hayo mawili umeongezeka na kutoa ujumbe kwa mataifa mengine umuhimu wa kutoa kipaumbele katika kushirikiana mataifa ya Kiafrika yenyewe.
Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa salamu za pole kwa Serikali na Wananchi wa Ghana kufuatia ajali ya ndege iliyotokea hivi karibuni na kusabibisha vifo vya watu nane ikiwemo Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mazingira wa nchi hiyo. Amesema Tanzania inaungana na Jamhuri a Ghana katika kipindi cha majozi na kuwaombea marehemu waweze kupumzika kwa amani.
Kwa upande Balozi wa Jamhuri ya Ghana nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mhe. Damptey Bediako Asare ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano aliopata kipindi chote alichohudumu kama balozi nchini. Amewasilisha salamu za Rais wa Ghana Mheshimiwa John Mahama ambazo amezitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa ujumla kwa kuendeleza ushirikiano na kuiunga mkono Ghana katika nyanja mbalimbali hususani katika majukwaa ya kimataifa.
Amesema hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hayati Kwame Nkurumah walitengeneza misingi ambayo nchi nyingi barani Afrika zimeendelea kuitumia katika kudumisha amani na umoja. Balozi Asare amesema ushirikiano huo unapaswa kuongezwa zaidi katika uchumi kwa manufaa ya mataifa yote.



Prev Post Raia wa Kigeni Akashutumiwa Baada ya Kumnywesha Tembo Bia
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook