

Dar es Salaam, Tanzania – Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, inatarajia kutoa hukumu Novemba 04, 2025 katika kesi ya jinai namba 48250 ya mwaka 2025, inayowakabili viongozi waandamizi wa CHADEMA, ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake wa Tanzania Bara, John Heche.
Kesi hiyo, inayosikilizwa chini ya Jaji Awamu Mbagwa, ilifunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed, pamoja na wenzake wawili. Washtakiwa wanatuhumiwa kukiuka amri ya Mahakama Kuu iliyotolewa Juni 10, 2025.
Wakili Jebra Kambole, mmoja wa mawakili wa utetezi, aliwaeleza wanahabari kile kilichojitokeza katika kesi hiyo siku ya Jumanne, Oktoba 28, 2025, Mahakamani hapo.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!