Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

PAMOJA NA KUFUZU..HUKO KIMATAIFA YANGA HAIKUWA KAZI RAHISI AISEE….UKWELI HUU HAPA…

  • 9
Scroll Down To Discover

HAIKUWA rahisi. Ndiyo, lakini mambo ndo kama mlivyosikia. Yanga imetinga hatua ya makundi kwa mara ya tatu mfululizo Ligi ya Mabingwa Afrika na ya nne mfululizo kwa michuano yote ya CAF ikiwa ni rekodi binafsi.

Yanga ilikuwa na kibarua kigumu baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 ugenini dhidi ya Silver Strikers juzi ikipindua meza kibabe kwa ushindi wa mabao 2-0 na kutinga hatua ya makundi.

Licha ya Yanga kufuzu hatua hiyo, ilikuwa na kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha inapata nafasi hiyo.

Nafasi nyingi walizotumia walishindwa kuzitumia na ushindi huo wa mabao 2-0 ndio uliamua hatma yao.

PRESHA ILIKUWA KUBWA

Kabla ya mchezo huo kulikuwa na presha kubwa kwa Yanga na sio kwa wachezaji pekee bali kwa viongozi na hata mashabiki wa timu hiyo kutokana na mshtuko wa kipigo cha ugenini.

Kipigo hicho hakikupita kirahisi kwani ililazimika Yanga kuachana na aliyekuwa kocha wake mkuu Romain Folz kutokana na matokeo hayo pia akilaumiwa tangu aichukue timu hiyo imekuwa haichezi kwa kuvutia.

PACOME NI YULE YULE

Kama kuna kitu Wanayanga wanaombea wakati wa mechi hasa zile ngumu, ni staa wao, Pacome Zouzoua asipate majeraha.

Katika mechi ya juzi Jumamosi, mashabiki waliofurika uwanja wa Benjamin Mkapa walikuwa roho juu baada ya staa huyo kuumia baada ya kuchezewa rafu iliyomfanya agaregare chini na kuwapa watu hofu.

Ndipo hapo dua zote zikaelekezwa kwake na hatimaye kurejea na kufanya yake ikiwamo kutupia bao la pili la ushindi baada ya lile yla Dickson Job.

Kiungo huyo raia wa Ivory Coast alifanya kazi kubwa kutengeneza hatari lango la wapinzani na aliamua kwa miguu yake na akili nguvu ya Yanga kwenda lango la Silver Strikers na haikuwa rahisi kumpokonya mpira ukiwa miguuni mwake labda aupoteze mwenyewe.

Alipeleka presha kwa wapinzani akicheza kwa kasi muda wote na kama Prince Dube angekuwa katika ubora basi angefunga mabao zaidi ya mawili kwa pasi nzuri alizotengenezewa na Pacome lakini mambo hayakuwa hivyo.

PENGO LA MZIZE/ DUBE AJIULIZE

Katika kitu ambacho mashabiki wa Yanga walikuwa wanatamani kukiona ni uwepo wa mshambuliaji wao, Clement Mzize aliyekosekana kwenye mchezo wa jana kwa kile kinachoelezwa ametonesha jeraha lake la goti.

Baada ya kikosi kutoka kila shabiki alihoji kukosekana kwake na wengi kuamini wamekosa mtu sahihi ambaye angepeleka presha kubwa kwa wapinzani, kwani Dube hakuwa na maajabu langoni licha ya kutengenezewa nafasi nyingi.

Mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita alifunga mabao 13 hakuwa na siku nzuri kazini hadi mwenyewe kuomba kufanyiwa mabadiliko.

UTIMAMU WA MWILI UPO CHINI

Yanga ya misimu minne ya ubora inapoteza mvuto, ndivyo unaweza kusema kutokana na namna timu hiyo inavyocheza huku mashabiki wakiwa hawana furaha kutokana na kile wanachokiona.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu juzi licha ya kuanza kwa kasi dakika 15 za kwanza na kupata bao la mapema dakika ya sita kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda pumzi ilianza kukata na kujikuta wakiingia kwenye mtego wa Silver Strakers kwa kucheza mpira wa taratibu.

Kipindi cha pili timu hiyo ilibakiwa na wachezaji wachache wenye utimamu wa mwili ambao walikuwa wanaonekana muda wote wakiipambania nembo ya Yanga huku Silver Strekars ikionyesha uhai kwa kushambulia zaidi lango la wapinzani.

Safu ya ulinzi na kipa Diarra ndiyo ilionekana kupata kazi ya kufanya kwani kipindi cha kwanza mipira mingi ya wapinzani iliishia eneo la kiungo lakini kipindi cha pili walijaribu kuingia mara kwa mara eneo la 18 ya Yanga na baadae kupata kona ambazo hata hivyo hazikuwa na madhara.

DUKE, DOUMBIA MTEGO

Jina la Moussa Bala Conte kutoka CS Sfaxien ya Tunisia linazidi kupotea mdogo mdogo midomoni mwa mashabiki wa Yanga.

Ndiyo, ni kutokana na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara, pia uwepo wa Duke Abuya na Mudathir Yahya.

Abuya alifanya kazi kubwa mbele ya mabeki wa kati na alitibua vikali mashambulizi ya wageni lakini akitibua hesabu nyingi za fundi wao Uchizi Vunga.

Uchizi alikutana na wakati mgumu kwenye mchezo huo na mpaka anatoka kwa mabadiliko, ilionekana mechi imekuwa ngumu kwake na shujaa ni huyu Mkenya Abuya ambaye hasifiki ila kazi yake ilikuwa kubwa.

Licha ya Abuya kucheza vizuri lakini bado Yanga inahaja ya kuwa imara zaidi eneo hilo la kati ili kuleta muunganiko mzuri kati ya viungo wa mbele na wale wakabaji.

Pia kulikuwa na Mohammed Doumbia alikichafua eneo la kati ambalo alikuwa anazurura kila upande na Mudathir Yayha ambaye mpira ulimshinda dakika 23 za mchezo na kuomba kutoka.

Kikosi cha Yanga kilikuwa bora eneo la kiungo, kila mchezaji katika eneo hilo alifanya kazi yake kwa usahihi na kuwapoteza wapinzani ambao wana falsafa ya kupigiana pasi fupi fupi na walipata mtihani wa kupenya eneo hilo, wakisaidiwa pia na mabeki Job na Ibrahim Hamad ‘Bacca’.

MABEDI KAUTUA MZIGO

Kocha wa muda Patrick Mabedi amemaliza kibarua chake salama baada ya kuivusha timu hiyo kwa ushindi huo huku pia kikosi hicho kikitawala mchezo licha ya presha kubwa.

Inawezekana Yanga isionyeshe kuna kitu kikubwa ambacho amekiongeza kocha huyo raia wa Malawi lakini kuwatuliza wachezaji wake na kucheza kwa nidhamu mbele ya Silver Strikers ambayo ilikuwa inaonyesha utulivu mkubwa, sio jambo linalotakiwa kupuuzwa.

Kaimu kocha huyo mkuu amesema timu ilikuwa bora na imeonyesha mabadiliko makubwa tofauti na mchezo wa awali lakini hajaridhishwa na walivyocheza kwa jumla.

“Timu ilikuwa bora dakika 15 za kwanza, napongeza wachezaji kwa kuivusha hatua ya makundi, lakini kipindi cha pili hatukuwa bora. Tunarudi uwanja wa mazoezi kujipanga vizuri tayari kwa mechi zinazofuata,” amesema na kuongeza;

“Kulikuwa na utofauti mkubwa wa kiuchezaji kati ya mechi iliyopita ugenini na ya nyumbani, kila mmoja ameona na ndiyo maana tumepata matokeo, nawapongeza wachezaji, benchi lote la ufundi na uongozi kwa ushirikiano mzuri kuanzia mwanzo wa maandalizi hadi kuhitimisha jambo letu la kutinga hatua inayofuata.”

Nahodha wa Yanga, Job amesema haikuwa rahisi kwa juhudi na kuipambania klabu na kwa pamoja wamefanikisha kutinga hatua ya makundi lengo ambalo waliliweka tangu mwanzo wa msimu.

“Mchezo ulikuwa mgumu na mzuri, tunashukuru Mungu tumefanikiwa. Tunawashukuru pia mashabiki waliojitokeza kwa wingi kutupa sapoti, ushindi unaenda kwao na tunawaahidi kuwa bora zaidi mechi zijazo wasiache kuja.”

The post PAMOJA NA KUFUZU..HUKO KIMATAIFA YANGA HAIKUWA KAZI RAHISI AISEE….UKWELI HUU HAPA… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KWA MIFUMO HII 3 YA KIMAFIA YA KOCHA MPYA YANGA….KUNA TIMU ITAKULA TENA 5😁😁…
Next Post Makala maalum ya uchaguzi Tanzania, katika Dira ya Dunia TV
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook