Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mpina Arejesha Fomu za Urais ACT-Wazalendo Baada ya Uamuzi wa Mahakama

  • 1
Scroll Down To Discover

Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Joelson Mpina, leo Jumamosi Septemba 13, 2025, amerejesha rasmi fomu yake ya kugombea urais katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) zilizopo Posta, jijini Dar es Salaam.

Mpina aliwasili akiwa ameambatana na mgombea mwenza wake, Bi. Fatma Ferej, na viongozi waandamizi wa chama hicho, akiwemo Kiongozi wa Chama Dorothy Semu, Mwanasheria Mkuu wa ACT-Wazalendo Omar Shaaban, pamoja na mgombea ubunge wa Jimbo la Temeke Sheikh Ponda Issa Ponda na Naibu Katibu wa Uenezi Taifa Shangwe Ayo.

Kurejeshwa kwa fomu hizo kunakuja baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma uliotolewa Septemba 11, 2025, ambao uliamuru mchakato wa Mpina kuendelea. Mahakama ilieleza kuwa utaratibu wa awali uliotumika kumzuia mgombea huyo haukuwa sahihi, hivyo kumpa fursa ya kurejesha fomu zake kama wagombea wengine.

Hatua hii inamweka Mpina rasmi kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya ACT-Wazalendo kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

MAKONDA ALIVYOSHANGILIWA na WANANCHI ARUSHA BAADA ya NCHIMBI KUMYANYUA na KUZINDUA KAMPENI ZAKE…



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 13, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook