
Dar es Salaam, Agosti 15, 2025 – Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo, amefanya ziara ya kushirikiana na kushuhudia shughuli za mabanda ya taasisi mbalimbali mara tu alipowasili kwenye Kongamano la Biashara – Kariakoo Festival 2025, lililofanyika leo katika soko la Kariakoo, Jijini Dar es Salaam.
Ziara ya Waziri Jafo ilikuwa fursa ya kuangalia kwa karibu bidhaa, teknolojia na huduma zinazotolewa na washiriki, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza biashara ndogo na za kati na kuchangia ukuaji wa uchumi wa ndani.
Kariakoo Festival ni kongamano linalojumuisha biashara, burudani na maonesho ya bidhaa, likilenga kuunganisha wadau wa biashara, wajasiriamali, na wananchi katika tukio la kipekee la maendeleo ya kiuchumi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!