Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Maendeleo  Ya Elimu Ni Mkombozi Wa Taifa Lolote  Duniani, Waziri Mkuu

  • 37
Scroll Down To Discover

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa maendeleo katika sekta ya elimu ndio mkombozi na mafanikio ya Taifa lolote duniani.
Amesema kwa kutambua hilo, uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliamua kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora katika ngazi zote.
Amesema hayo wakati alipozungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Ruangwa mkoani Lindi, wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa iliyofanyika mwaka 2025.
“Mliopo shuleni na mnaokuja, tambueni kuwa tuna maeneo muhimu ya kuwaelimisha, mtapata elimu iliyobora na imara itakayowapa maarufa na ujuzi ili muweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi”
Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imefanya maboresho ya mitaala kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi yaliyopo duniani ikiwemo mahitaji makubwa ya ajira kwa vijana.
“Mabadiliko haya yameifanya mitaala yetu itakayofundishwa shuleni kila mwanafunzi akimaliza ana uwezo wa kutumia mazingira alimo na taaluma aliyonayo kuyabadilisha kuwa uchumi”
Akisoma matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2025, Makamu Mkuu wa Shule Amon Chalamila hiyo amesema kuwa shule hiyo ilisajili wanafunzi 188 ambapo wote walifanya mitihani na wanafunzi 90 walipata daraja la kwanza, wanafunzi 95 walipata daraja la pili, wanafunzi watatu walipata daraja la tatu na hakuna mwanafunzi aliyepata daraja na nne na sifuri. “Ufaulu huu ni sawa na GPA ya 2.34”.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI LEO AGOSTI 06, 2025
Next Post Tanzania Yatoa Wito Kwa Washirika Kutimiza Ahadi Zao Kwa Maendeleo Ya Nchi Zisizo Na Mlango Wa Bahari
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook