Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mpox Yasambaa Magharibi mwa Kenya, Vifo Viwili Vyaripotiwa Busia

  • 42
Scroll Down To Discover

Ugonjwa wa Mpox Wasambaa Kenya Magharibi mwa Kenya sasa ndio kitovu cha mlipuko wa ugonjwa wa Mpox huku kaunti za Busia, Bungoma na Kakamega nchini humo zikithibitisha kuwa na wagonjwa kadhaa walioambukizwa ugonjwa huo unaosababishwa na virusi.

Kaunti ya Busia ni eneo la pili lililoathiriwa zaidi nchini Kenya huku kukiwa na maambukizi 56 yaliyothibitishwa na vifo viwili vilivyoripotiwa hadi sasa.

Mamlaha za afya katika kaunti ya Busia zimeanzisha zoezi linaloongozwa na Timu ya Usimamizi wa Afya ya Kaunti (CHMT), linalolenga kuzuia kuenea kwa virusi.

Evans Shiraku Mratibu wa uchunguzi wa ugonjwa wa Mpox, ambaye alihutubia washikadau wakati wa kongamano la uhamasishaji lililofanyika mapema wiki hii alisema kuwa kaunti haiwezi kusalia kimya kutokana na mlipuko huo.

Data taifa za karibuni zinaonyesha kuwa Kenya imethibitisha kesi 226 za Mpox katika kaunti 13 nchini. Kaunti ya Busia ina wagonjwa 56, 2 wakiwa wamelazwa hospitali, vifo viwili na wagonjwa 8 wanapatiwa matibabu nyumbani.

Hata hivyo mratibu wa uchunguzi wa ugonjwa wa Mpox amesema kuwa moja ya wasiwasi mkuu uliopo ni namna kaunti ya Busia ilivyo karibu na Uganda; na hivyo kuibua hatari ya kuongezeka maambukizi ya kuvuka mpaka.

Kati ya kesi zilizothibitishwa hadi sasa, 53 ni raia wa Kenya, na watatu ni Waganda.



Prev Post Raila Odinga: Handshake Haikuwa ya Maslahi Binafsi, Sikutegemea Chochote
Next Post Waziri Bashungwa Amwakilisha Rais Samia Mkutano Wa Wakuu Wa Nchi 
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook