Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Adaiwa Kumuua Mama Mkwe Kwa Kumkata Mapanga

  • 34
Scroll Down To Discover

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Jumanne Mabodo (30) kwa tuhuma za kumuua mama mkwe wake Kabula Masanja (50) kwa kumkata kwa panga nyumbani kwa marehemu, kijiji cha Chumwi, Wilaya ya Musoma, Julai 19, 2025. Binti wa marehemu, ambaye ni mke wa mtuhumiwa, alijeruhiwa na anaendelea na matibabu. Chanzo ni mgogoro wa kifamilia baada ya mke wa mtuhumiwa kudai kuwa mumewe ni mwizi.

Katika tukio jingine, Marwa Mgesi (17) wa Mugumu Serengeti, alikamatwa na silaha aina ya pisto yenye risasi 4 aliyomwibia bosi wake huko Monduli, Arusha.

Polisi pia wanachunguza kifo cha Nyangige Matiku (44) wa Mtukula, Butiama, aliyedaiwa kujinyonga kutokana na wivu wa mapenzi.

Jeshi la Polisi limewaasa wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama na kuepuka kujichukulia sheria mkononi.



Prev Post Watumishi Wawili wa TRA Wafariki Katika Ajali Geita
Next Post Bangladesh Yaomboleza Baada ya Ajali ya Ndege Kuwaua 27, 88 Wajeruhiwa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook