

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 5, 2025 ameshiriki katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Kanisa la Arise and Shine, iliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe – Dar es Salaam.
Katika tukio hilo lililohudhuriwa na maelfu ya waumini na viongozi mbalimbali wa dini, serikali na taasisi binafsi, Rais Samia alipokelewa kwa furaha na heshima kubwa, huku akitoa hotuba iliyojaa busara, mshikamano wa kitaifa na ujumbe wa amani.
Rais amelitakia kanisa hilo kila la heri katika safari yake ya kiroho na kijamii, akisisitiza umuhimu wa taasisi za kidini katika kuimarisha maadili, upendo na mshikamano wa kijamii, pamoja na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.
Viongozi wa Kanisa hilo wamemshukuru Rais kwa kuwa kiongozi wa kwanza wa kitaifa kuhudhuria tukio la aina hiyo, na wamempongeza kwa juhudi zake katika kuimarisha uhuru wa kuabudu na kuendesha Taifa kwa hekima.



Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!