

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini ( TAA) imetoa wito kwa wananchi kuendelea kuiamini mamlaka hiyo katika usimamizi na uendelezaji wa viwanja vya ndege 61 nchini katika utoaji wa huduma zake za usafirishaji wa abiria ndani na nje ya Nchi.
Kauli hiyo imeyotolewa Jijini Dodoma na Meneja wa uendeshaji kiwanja cha ndege cha kimataifa Msalato Jeff shantie katika maadhimisho ya kitaifa ya wiki ya Maonesho ya utumishi wa umma.
Ameeleza kuwa lengo mamlaka hiyo ambayo ilianzishwa kwa mujibu wa sheria namba nane ya mwaka 2024 kwa kusudi la kusimamia viwanja vya serikali vya tanzania bara .
Aidha amesema ushiriki wao katika maonesho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi namna mamlaka hiyo inavyowajibika katika kuleta mafanikio ya mamlaka hiyo katika usimamizi wa viwanja.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!