Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

KISA CAF….HAYA HAPA MAAMUZI MAGUMU YA MO DEWJI SIMBA….FADLU KICHEKO TU…

  • 26
Scroll Down To Discover

BILIONEA wa Klabu ya Simba, Mohammed ‘MO’ Dewji ameridhishwa na mafanikio ya timu hiyo kimataifa licha ya kwamba imeshindwa kubeba ubingwa wa Afrika kwa mara nyingine na fasta ameamua kufanya jambo moja linaloweza kuwapa furaha Wekundu wa Msimbazi.

Bilionea huyo amempongeza kocha mkuu wa timu hiyo, Fadlu Davids aliyekutana naye katika kikao kizito na kumhakikishia usajili kwa ajili ya msimu ujao utakuwa mzito na kumfanya kocha huyo kukubali kutuliza akili na kusalia Msimbazi ili kuzidi kuijenga timu hiyo.

Ipo hivi. Kabla ya Simba kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kukwama kubeba ndoo mbele ya RS Berkane ya Morocco, kulikuwa na ofa zilizoanza kumiminika kwa Fadlu kutoka klabu kadhaa zikiwamo za nchi anayotoka ya Afrika Kusini.

Hata hivyo, MO Dewji amemzuia kusepa kwa kumpa mkataba mpya kutokana na kuridhishwa na namna alivyoutumia msimu wa kwanza kuirudisha Simba katika ubora na ushindani mkubwa uwanjani katika Ligi Kuu na hata michuano ya kimataifa akiifikisha fainali hizo za CAF.

Taarifa kutoka ndani ya Simba ni kwamba MO amempongeza Fadlu kwa hatua ambayo kikosi cha timu hiyo kimefikia hadi sasa ikilikosa kidogo taji hilo la shirikisho, huku ikiendelea kusalia kuchukua mataji moja la Ligi Kuu Bara huku wakilikosa tena Kombe la Shirikisho (FA) baada ya Jumamosi iliyopita kupoteza nusu fainali na Singida BS.

MO amemtaka Fadlu aendelee kusalia kikosini ili kuifundisha timu hiyo, huku akimhakikishia usajili mzito wa hatua ya tatu katika kukiboresha kikosi hicho.

Inaelezwa Fadlu amemwambia bilionea huyo kuwa anahitaji mastaa wapya wa maana watakaokuja kuongeza nguvu katika kikosi hicho kabla ya kuanza mashindano ya msimu ujao ambapo timu hiyo itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika iliyoikosa msimu huu.

“MO (Dewji) amekutana na Fadlu na amefurahishwa sana na hatua ya kikosi ilipofikia, hii sio mara ya kwanza, aliwahi kumpongeza kabla, lakini baada ya fainali hii ya Zanzibar ya Kombe la Shirikisho wamezungumza tena na amemwambia ana furaha na namna timu ilivyofikisha,” alisema bosi huyo wa juu ndani ya Simba na kuongeza;

“Kwa sasa wamekubaliana kwamba usajili mkubwa utafanyika kama ambavyo kocha aliomba na kuna mapendekezo yake yanaendelea kufanyiwa kazi kwa kasi kubwa. Hatua hii imemfanya Fadlu kumwambia MO kwamba hana mpango wa kuondoka kwasasa na anataka kuendeleza zaidi mradi ambao waliuanza msimu huu.”

Fadlu bado ana mkataba wa mwaka mmoja baada ya kusaini dili la miaka miwili, wakati anatua Simba akitokea Raja Casablanca ya Morocco aliyotwaa nayo ubingwa wa Ligi Kuu ya nchini humo na sasa MO anataka kuurefusha zaidi mkataba huu kabla ya kuanza msimu ujao.

MATOLA NDANI

Mbali na Fadlu, taarifa zaidi zinasema kuwa, makocha wasaidizi wa timu hiyo akiwamo Seleman Matola nao wapo katika mazungumzo ya kuongezwa kwa mikataba yao kwa nia ya kuendeleza moto wa benchi hilo la ufundi kwa manufaa ya Simba ndani na nje ya nchi.

Matola mkataba alionao unaisha na yupo mbioni kuongeza akizima tetesi za kutaka kunyakuliwa na Tanzania Prisons, huku wasaidizi wengine wa Fadlu nao wakiwa pia kwenye mazungumzo ili kuongezewa mikataba waliyonayo.

Credit:- MwanaSpoti

The post KISA CAF….HAYA HAPA MAAMUZI MAGUMU YA MO DEWJI SIMBA….FADLU KICHEKO TU… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post ZA NDAAANI…MOKWENA AIPA MASHARTI HAYA YANGA….MFARANSA WA ASEC MHHH 🧐….
Next Post Fiston Mayele Aandika Historia: Amaliza Ukame wa Pyramids FC kwa Kutwaa Taji la Ligi ya Mabingwa Afrika
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook