
MAGAZETI ya Leo Jumamosi 31 May 2025
MAGAZETI ya Leo Jumamosi 31 May 2025
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2025 iliyozindiliwa jijini Dodoma May 30,2025 katika ukurasa wake wa 41, 42, 43, na 44 imetaja mkakati wa kuendelea kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji nchini.
Mipango iliyopo ni kuunganisha kwa kiwango cha lami barabara za makao makuu ya mikoa na wilaya.
Kuhakikisha kuwa barabara zote za vijijini zinakarabatiwa na kujengwa, ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.
Kuanza ujenzi wa barabara za juu (flyovers) katika makutano ya barabarabkatika maeneo ya Morocco, Mwenge, Magomeni na Tabata, jijini Dar es Salaam.
Kukamilisha miradi ya ujenzi wa madaraja inayoendelea ikiwemo madaraja ya Malagarasi Chini (Kigoma), Mkenda (Ruvuma), Godegode (Dodoma), Mzinga (Dar es Salaam), Simiyu (Mwanza), Nzali (Dodoma), Ugalla (Kigoma), Sanza (Singida), Mitomoni (Ruvuma), Malagarasi Juu (Kigoma), Mkundi (Morogoro), Pangani (Tanga), Kalebe (Kagera), na Mto Msimbazi eneo la Jangwani (Dar es Salaam).
Ujenzi wa barabara kubwa za kuunganisha mikoa na nchi jirani ikiwemo barabara ya njia nne ya Igawa – Uyole – Songwe – Tunduma (km 218), barabara ya Kibaoni – Majimoto – Inyonga (km 162), barabara ya Tarime – Mugumu (km 87), barabara ya Geita – Bukoli – Kahama (Busoka) km 133.9, barabara ya Mabokweni – Maramba – Bombo Mtoni – Umba hadi Same (278km).
Kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya IV – VI katika barabara za Ali Hassan Mwinyi – Morocco – Mwenge – Tegeta na Mandela kuanzia makutano ya Ubungo na Bandari, makutano ya Mandela/ Tabata – Tabata Segerea na Tabata – Kigogo.
Ujenzi wa reli ya Standard Gauge Mwanza – Isaka (km 341), Makutupora – Tabora (km 368), Tabora – Isaka (km 165), TaboraKigoma (506), Uvinza- Musongati (km 156.6)
Kujenga reli na kuweka usafiri wa treni za mijini (Metro) katika majiji ya Dar es Salaam na Dodoma ili kupunguza msongamano na kurahisisha usafiri
Kujenga reli ya kisasa ili kuunganisha Bandari ya Tanga kuelekea Arusha hadi Musoma (km 1,108)
Kujenga bandari mpya ya Bagamoyo Kuboresha bandari za Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Kigoma, Kalema, Musoma na bandari kavu katika eneo la Kurasini – Dar es Salaam, Kwala – Pwani na Ihumwa – Dodoma.
Kukarabati meli zilizopo katika maziwa makuu na kujenga meli mpya za mizigo na abiria katika Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa na Bahari ya Hindi.
Kuendelea kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania kwa kununua ndege nane.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!